Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey amefanyiwa upasuaji kuunga sehemu ya chini ya mguu wake wa kulia uliyovunjika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stoke siku ya Jumamosi.
Ramsey mwenye umri wa miaka 19 anayechezea pia timu ya taifa ya Wales alitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuchezewa rafu na mlinzi wa Stoke Ryan Shawcross, aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu huku akibubujikwa na machozi akijutia kosa hilo.
Taarifa iliyotolewa na klabu ya Arsenal kupitia mtandao wake imesema upasuaji aliofanyiwa Ramsey siku ya Jumamosi ulikwenda vizuri, lakini hajafahamika lini atapona kabisa.
Kwa muda uliosalia kumalizika msimu huu Ramsey hataweza kucheza soka.
Baada ya mchezo wa siku ya Jumamosi, meneja wa Arsenal, Arsene Wenger ameielezea rafu aliyochezewa Ramsey "haukubaliki kabisa".
Lakini baadae Shawcross alielezea masikitiko yake kwa Ramsey na akasema katika taarifa yake rasmi, hakukusudia kumuumiza kwa makusudi kutokana na rafu aliyocheza.
Ameongeza kusema: "Kamwe sina tabia ya kumuumiza mchezaji mwenzangu. Nimeuzunishwa Aaron ameumia vibaya na ninamuombea apone haraka"Pata kideo jinsi alivyoumia.